Joka la mdimu uhakiki pdf | uhakiki wa riwaya ya Joka la mdimu notes | Joka la mdimu download pdf | Joka la mdimu uhakiki videos | Joka la mdimu uhakiki age Joka la mdimu dhamira pdf | Joka la mdimu video | Joka la mdimu pdf notes download
Fani katika riwaya ya joka la mdimu
MWANDISHI: ABDALLAH J. SAFARI
- Sura ya kwanza, MINDULE:Hapa mwandishi anatueleza kuhusu habari za Amani dereva Taxi, masaibu anayopata katika kazi yake kutokana na uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta.
- Sura ya pili, TINO:Hapa tunaelezwa kuhusu maisha ya Tino na kazi anazofanya ya kuvuta kwama. Tunaambiwa kuhusu hali ngumu ya maisha ya Tino na wakazi wengine wa Sega, hapa tunaelezwa pia kuhusu masuala ya uongozi jinsi ulivyo mbovu na ugawanywaji mbovu wa vyanzo vya uchumi na bidhaa.
- Sura ya tatu, JINJA MALONI:Katika sura hii tunaelezwa kuhusu maisha ya Jinja Maloni, hapa anaibua dhamira kama vile za uvamizi, uhalifu na mauaji pia anaendela kutueleza kuhusu hali ngumu ya maisha.
- Sura ya nne SEGA:Maisha ya wakazi wa Sega yanaelezewa hapa jinsi yalivyo ya dhiki, pia tunaelezwa kuhusu Tino na mkewe maisha yao yalivyo na familia yao, anaibua dhamira ya mapenzi ya dhati na upendo kwa familia.
- Sura ya tano, BOKO:Hapa tunaelezwa kuhusu adha ya usafiri kwa watu, shida ya mafuta, ubovu wa miuondmbinu kama vile barabara, vinasemwa hapa.
- Sura ya sita, BROWN KWACHA:Sura hii inaeleza habari za Brown maisha yake na tabia zake, anaibua dhamira kama vile uhujumu uchumi, biashara za magendo, suala la kutowajibika kwa watumishi, suala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa na mapenzi ya pesa ambapo sifa zote hizi alizibeba Kwacha.
- Sura ya saba, KWALE:Hapa yanaelezwa mambo kuhusu hifadhi ya Kwale, safari ya Brown na Leila kwenda kutembea kwale. Hapa yanatajwa mambo ya udhalimu wa kuharibu mali za umma (maliasili za taifa) mfano pembe za ndovu, vipusa pia mapenzi yasiyo ya kweli.
- Sura ya nane, DAKTA MIKWALA:Dakta Mikwala ndiye mhusika mkuu anayeelezwa hapa, tunalezwa juu ya ugumu wa upatikanaji wa huduma za afya kwani Cheche anashindwa kutibiwa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.
- Sura ya tisa, CHECHE:Tunaelezwa juu ya juhudi za Amani na Tino ili kumsaidia Cheche aweze kwenda kutibiwa Uingereza. Wanafanikiwa kupora benki na kupata pesa za kumtibu Cheche.
- Sura ya kumi, MOTO:Hapa hatma ya visa vidogo vidogo imeelezwa kwa kutolewa hatma ya maisha ya Cheche na Brown Kwacha. Cheche alipata matibabu na kupona na Browna anafanikiwa kuirubuni serikali kwa kuipanga mahesabu ya uongo.
- Matumizi ya nafsi ya tatu Umoja. Imetawala: Mfanouk.5“Amani aliangalia…….” Uk.25 “Amani alijizuia” .Nafsi ya tatuwingi;mfano uk. 63“ wote walitoka nje kuelekea klabuni”.Piauk.53 “wale wanaume walimvamia”
- Matumizi ya nafsi ya pili: Mfanouk.106 “ mmechoka kuangalia video?” “aa tumeshaziona mara nyingi tunaombaainanyingine.” Mazungumzo baina ya mke wa Brown na wanae.Pia mazungumzo baina ya Brown na Leila.Uk.113. “habari za asubuhi”“ Nzuri sijui wewe” alijibu“Uliota njozi njema?”"Wapi?""Kwa nini?"
- Matumizi ya nafsi ya kwanza: Mfanouk. 39 “mimi nimemaliza” “….kuiba nimeiba sana….”
- Matumizi ya nyimbo.Uk.70. wimbo wa Chaupele: “Chaupele mpenzi, haya usemayoKama ni maradhi, yapeleke kwa DaktariWanambia niache rumba,na mimi sikuzoeaSitaweza kuliacha rumba, kwa sababu yakoKama wanipenda, nenda kwa baba”Piauk.58 “sega! Sega! Sega!, usioogope” wimbo waliouimba washabiki wa michezo.
- Masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi: Hapa mwandishi amemtumia muhusika kusimulia kisa kingine kidogo ndani ya kisa kikuu. Mfanouk.39mhusika Tino anamsimulia mteja wake maisha yake ya mwanzo kabla hajaanza kazi ya kuvuta kwama.
zinazohusiana
- Tashibiha:Uk.117 “ngozi yake nyeusi kama udongo wa mfinyanzi”Uk.122 “mweusi kama sizi la chungu”Uk.9 “Zepher 6 ile iliunguruma kama simba dume”Uk.10 “mteuzi mithili ya Mbega”Uk.35 “……miguu yake ikakazana mithili ya upinde uliotaka kufyatuliwa”
- Sitiari:Uk.91 “Brown Kwacha alikuwa kinyonga”Uk.15 “sarahange wetu mboga kweli siku hizi”Uk.40 “huku twakaa vinyama vya mwitu”Uk.72 “sote ni kobe”
- Tashihisi:Uk.109 “……gari lile zuri lilioondoka kwa madaha” Uk.143 “ kuta nyeusi za nyumba zaidi ya kumi zilisimama twe!kuomboleza” Uk.91 “pua zake zikalakiwa na riha na ashrafu ya manukato”;Uk.12 “utumbo ulimlaumu”; Uk.27 “mvua ikapiga kwa kiburi na kuviadhibu vibati vibovu”.
- Tafsida:Uk. 49 “isijekuwa nimekukatiza haja!”,piauk.hohuo“kinyesi”.
- Takriri:Uk.151 “mwizi! Mwizi! Jambazi! Jambazi!”Uk.57 “shinda! Shinda! Shinda!”Uk.33 “karibu baba, kariibu kaka, karibu mkwe” Uk.72 “uhuru upi? Uhuru gani? Uhuru wa nini na nani?”
- Mdokezo:Uk.149 “lakini……..”
- Onomatopea au tanakali sauti:Uk. 1 “saa mezani niliendelea kugonga taratibu ta! ta! ta!”; Uk.10 “ikatoka sauti kali tupu ta nye nye”;Uk.67 “upepo wa stova uliolia shshsh”;
- Tashtiti:Uk.113. leila anamuuliza Brown maswali ambayo anayajua majibu yake. Brown:“uliota njozi njema? Leila: Wapi?” Leila:Kwanini? Brown:Mwenywe unajua”
- Nidaa:Uk.39 “Aaa! Limbukeni wa jiji anataka kunitia kashkash”: Uk 30 “nguo zangu Mungu wee!” Uk.42 “Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiunna!” Uk.92 “Ah! Leila kwacha alimsalimia kwa furaha” Uk. 105 “Lahaula”
- Methali:Uk.78 “asilojua mtu ni usiku wa kiza”Uk.83 “ukiona mwenzako anyolewa zako tia maji”Uk.98 “mtaka waridi sharti avumilie miiba”Uk. 99 “biashara haigombi”Uk.43 “ajizi nuksani huzaa mwana kisirani”
- Misemo:Uk.10 “asiye na bahati habahatishi”Uk.47. “asiyezika hazikwi”Uk.64 “mmetupa Jongoo na mtiwe”Uk.98 “asali haichomvwi umoja”Uk.111 “ajali haina kinga”Uk.115 “mwenye macho haambiwi tazama”Uk.120 “matendo hushinda maneno”Uk.47. “asiyezika hazikwi”
- Nahau:Uk.11 “sio unanilalia kila mara” –kunidhulumuUk.107 “alikonda akajipa moyo” –kujifariji moyo
- Ni dereva taxi
- Ana upendo wa dhati
- Ni mchapakazi
- Ana hekima na busara
- Ana huruma
- Ni rafiki wa kweli wa Tino
- Kutokana na hizo sifa amani ni mhusika bapa
- Anafaa kuigwa na jamii
- Ni mchapakzi
- Mlezi bora wa familia
- Baba wa Cheche
- Ana huruma
- Ana upendo wa dhati
- Ni makini
- Ni jasiri
- Ni mwanamichezo
- Anafaa kuigwa na jamii
- Ni mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni
- Ni muhuni na Malaya
- Fisadi na mla rushwa
- Anafanya biashara haramu
- Hana mapenzi kwa familia yake
- Anapenda anasa
- Si muaminifu kwa mkewe
- Si muadilifu
- Hafai kuigwa na jamii
- Ni mhusika bapa
- Ni jasiri na mwenye nguvu
- Ana huruma na upendo
- Mchapakzi
- Mlevi
- Maskini
- Ni mhusika duara
- Ni daktari bingwa wa mifupa
- Anapenda rushwa
- Si muwajibikaji katika kazi yake
- Ni mlevi
- Hafai kuigwa na jamii
- Ni mhusika bapa
- Ni mfanyabiashara
- Ni mtoa rushwa
- Ana biashara za magendo
- Rafiki wa Brown
- Hafai kuigwa na jamii
- Ni mhusika bapa
- Ni mfanyakazi bandarini
- Ni mwanamichezo
- Ni jasiri ana kipato duni
- Rafiki wa Tino na Aman
- Ni mtoto wa Tino
- Ana nidhamu na bidii
- Ni mwanamichezo
- Ana upendo kwa wazazi wake
- Ni mtiifu na msikivu
- Mcheshi na mudadisi
- Alivunjika kiuno michezoni
- Ni mhusika bapa
- Ni mke wa Tino
- Mvumilivu
- Ana mapendo ya dhati kwa familia yake
- Ni mchapakazi
- Ni mhusika bapa
- Wasichana wahuni waliojiuza kwa Brown Kwacha
- Hawafai kuigwa na jamii
Kumbuka! pdf ya bure inaweza kuwa na pasword hoivyo basi baada ya kudownload ni vyema ukajiunga na magroup yetu na kuomba password ya file husika
Joka la mdimu uhakiki pdf | uhakiki wa riwaya ya Joka la mdimu notes | Joka la mdimu download pdf | Joka la mdimu uhakiki videos | Joka la mdimu uhakiki age Joka la mdimu dhamira pdf | Joka la mdimu video | Joka la mdimu pdf notes download