uhakiki wa tamthiliya ya kilio chetu pdf download | dhamira katika tamthiliya ya kilio chetu pdf | Tamthiliya ya kilio chetu full movie download | kitabu cha kilio chetu kidato cha tatu pdf |
tamthiliya ya kilio chetu full movie | Tamthiliya ya kilio chetu video download | migogoro katika tamthiliya ya kilio chetu | kilio chetu sehemu ya kwanza | kilo chetu medical aid foundation | dhamira za kilio |
uchambuzi wa tamthiliya ya kilio chetu
TAMTHILIYA; KILIO CHETU
MWANDISHI; MEDICAL AID FOUNDATION
MCHAPISHAJI; TANZANIA PUBLISHING HOUSE
MWAKA; 1995
Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii
katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya
kijinsia.
Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko
na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho
suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya
kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho
ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa.
FANI
MUUNDO
Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kutuonesha
wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho Joti
mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi.
Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI.
Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita.
sehemu ya kwanza. Inaonesha jinsi ambavyo gonjwa la UKIMWI linaiteketeza, jamii
wengi wao wakiwa watoto ambao hawakuwa na elimu ya jinsia na
mahusiano.
sehemu ya pili. Wazazi wanabishana juu ya kuwapatia elimu ya jinsia na mahusiano
watoto wao. Mama Suzi anasema jambo hilo liko kinyume na maadili, lakini
Baba Anna yeye anaunga mkono suala hilo.
sehemu ya tatu. Inaeleza kuhusu watoto Joti na Suzi ambao wamekwisha anza mambo
ya ngono. Pia watoto wameathiriwa na utandawazi kwani wanaangalia video
za ngono bila wasiwasi.
Sehemu ya nne. Inazungumzia tabia hatarishi za Joti kuwa na wasichana wengi.
Vilevile Anna kutokana na elimu ya jinsia na mahusiano aliyonayo,
anaendelea kukwepa vishawishi.
Sehemu ya tano. Mtoto Suzi kapata mimba, anabaki njia panda akiwa hajui afanye
nini.
Sehemu ya sita. Hii ni sehemu ya sita. Tunamuona Joti akifa kwa UKIMWI, na Suzi anabaki akiwa na mimba
pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
MTINDO
Tamthiliya hii imetumia mtindo wa;
i. Dayolojia – majibizano ya wahusika yametawala toka mwanzo mpaka mwisho
wa tamthiliya hii.
ii. Monolojia – mtindo huu wa masimulizi umetumika japo kwa kiasi
kidogo.
iii. Mtindo wa masimulizi ya ki ngano - mfano katika ukurasa wa 1 Mtambaji anasimulia,
“Hapo zamani za kale paliondokea kisiwa kimoja kikubwa sana. Kisiwa
kilikuwa na watu wa kila aina…”
Zinazohusiana
iv.Matumizi ya nyimbo – katika ukurasa wa 29, Anna anaimba wimbo unaokemea wanaume wanaomfuata kumlaghai.
“Anna, Anna, Anna mie niacheni mie x 2
Msichana mdogo bado ninasoma niacheni mie.”
v. Matumizi ya nafsi
Nafsi zote zimetumika lakini nafsi ya pili imetawala zaidi.
WAHUSIKA
JOTI
- Mhusika mkuu
- Hana elimu ya jinsia na mahusiano
- Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wasichana wengi. Wengine
wakiwa wakubwa kuliko yeye.
- Mwisho anakufa kwa UKIMWI
SUZI
- Mhusika mkuu
- Msichana mdogo anayesoma shule ya msingi
- Hana elimu ya jinsia na mahusiano
- Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzake Joti,
pia anaambukizwa UKIMWI na kupata mimba.
ANNA
- Msichana mwenye elimu ya jinsia na mahusiano
- Anakataa vishawishi vya wanaume kwa sababu anajitambua kwa sababu ya
kuwa na elimu ya jinsia
MAMA SUZI
- Anashikilia mila na tamaduni za zamani
- Haungi mkono kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano, anaamini
kufanya hivyo ni kuwaharibu watoto
MJOMBA
- Mwanaume mtu mzima
- Anaunga mkono wazazi kuwapatia watoto wao elimu ya jinsia na
mahusiano.
Wahusika wengine ni; Baba joti, Mama Joti, Baba Anna, Choggo, Mwarami, Jumbe, Chausiku,
Jirani, na wengineo.
MANDHARI
Mandhari ya mjini yametumiwa na mwandishi. Pia kunayo mandhari ya;
Nyumbani, kijiweni, barabarani, n.k
MATUMIZI YA LUGHA
Tamathali za semi
i. Tashibiha. “Wakapukutika kama majani ya kiangazi.” Uk 1
ii. Sitiari. “We mbwa mweusi.” Uk 10
iii. Takriri. “vikawazoa, vikawazoa… vikawazoa.” Uk 3
iv. Tanakali sauti. “pwi, pwi, pwi,” uk 18
v. Tafsida. “Kafa kwa kukanyaga nyaya.” Uk 4
vi. Mubaalagha. “mtu si mtu, kizuka si kizuka” uk 4
2. Misemo, nahau na methali
i. Msemo. “Wembamba wa reli treni inapita.” Uk 7
ii. Msemo. “Kukimbilia suti na nepi hujavaa.” Uk 28
iii. Methali. “umeula wa chuya.” Uk 29
iv. Methali. “shukrani ya Punda ni mateke” uk 19
v. Nahau. “nimekuvulia kofia” uk 6
3. Picha na taswira
“Dubwana” –ugonjwa wa UKIMWI;
“Nguru” –aina ya Samaki wabaya–amefananishwa na mtu mbaya;
MAUDHUI
DHAMIRA
Dhamira nyingi zimejadiliwa katika tamthiliya hii, miongoni mwa dhamira
hizo ni;
i. Elimu ya jinsia na mahusiano
Jamii imekumbwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili pamoja na maradhi hatari
yasiyotibika kama UKIMWI. Hivyo wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto wao
juu ya njia sahihi za kujikinga na matatizo haya. Katika tamthiliya
tunaona pande mbili, ule unaoshikilia ukale na upande unaotaka mabadiliko.
Baba Anna, anawaelimisha watoto wake juu ya madhara ya kujihusisha na
ngono katika umri mdogo, Anna anaelewa na anafanikiwa kukwepa vishawishi.
Hali ni tofauti kwa Mama Suzi anaamini kuwapatia watoto elimu ya jinsia na
mahusiano ni kuwaharibu na kuwapoteza. Anaposhauriwa kuwapatia watoto
elimu hiyo anafoka,
“Huko si ndiko kunifundishia wanangu umalaya? Umfunze mwanangu habari
za ngono…”
Kutokana na kutokukubali kuwapatia wanawe elimu hii, Suzi anapewa mimba
na kuambukizwa UKIMWI.
ii. Mmomonyoko wa maadili
Maadili hayazingatiwi tena katika jamii. Watoto kwa wakubwa wote
wamepotoka. Tunaona watu wazima wakitembea na watoto wadogo, mfano
Chausiku anamahusiano na mtoto mdogo Joti. Pia watoto wamejiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi, Joti anamahusiano na Suzi. Watoto hawahawa
wanaangalia video za ngono bila kuogopa chochote. Katika ukurasa wa 20 Joti anasikika akiwahamasisha wenzake.
“Yaap, ukimtaka Suzi, chukua. Picha ya ngono, matusi angalia!”
Mmomonyoko huu wa maadili utaondolewa endapo watoto watapatiwa
elimu.
iii. Athari ya sayansi na teknolojia
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mabadiliko makubwa katika
jamii, mfano katika tamthiliya hii, watoto wanakwenda kuangalia picha za
ngono na kuwafanya waharibikiwe kifikra kwa kutamani kuigiza kile
wanachokiona. Joti, mtoto kinara wa kutazama picha hizo anaambulia
UKIMWI na kufa angali mtoto mdogo.
iv. Nafasi ya mwanamke katika jamii
Nafasi ya mwanamke ni jumla ya mambo yote ayatendayo mwanamke katika
kazi ya fasihi. Mengine huwa mazuri yanayostahili pongezi na machache
huwa mabaya yanayostahili kukemewa kwa nguvu. Katika tamthiliya hii,
mwanamke amechorwa kama;
- Chombo cha starehe. Mfano Joti anamtumia Suzi kwa ajili ya
kujistarehesha.
- Asiyependa mabadiliko. Mama Suzi hataki kutoa elimu ya jinsia kwa
wanaye.
- Asiye na maadili. Suzi hana maadili, anajiingiza katika mahusiano ya
kimapenzi katika umri mdogo.
- Mwenye elimu na asiyedanganyika. Anna ana elimu ya jinsia na mahusiano,
wanaume wanashindwa kumdanganya kwa pesa na maneno matamu.
UJUMBE
i. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Suzi na Joti hawakufunzwa
vyema na wazazi wao, badala yake ulimwengu unawafunza.
ii. Elimu ya jinsia na mahusiano itolewe kwa watoto. Elimu hii itawafanya
waepuke vishawishi.
iii. Sheria kali zitungwe dhidi ya watu wanaowalaghai watoto. Kuna watu
wazima wanaowaingiza watoto katika vitendo vya kimapenzi kama Chausiku
anavyomlaghai Joti. Sheria kali itungwe na isimamiwe kuwakomesha.
iv. Wazazi wote washirikiane katika malezi ya watoto. Baba Anna na Mama
Anna wanashirikiana katika malezi ya watoto wao. Matokeo bora
yanaonekana.
MIGOGORO
Migogoro iliyojitokeza ni pamoja na;
Migogoro ya wahusika
i. Mgogoro wa Joti na Suzi
Mgogoro huu unasababishwa na tabia ya joti kuwa na mahusiano na wasichana
wengi. Suluhisho la mgogoro huu ni Joti kumuomba msamaha Suzi.
ii. Mgogoro wa Suzi na Mama yake
Mgogoro huu unasababishwa na mama Suzi kuvikuta vidonge vya kuzuia mimba
katika sketi ya mwanaye. Suluhisho la mgogoro huu ni Mjomba kumwamuru Suzi
aende ndani na mazungumzo kati ya Mjomba, Mama Suzi na majirani wengine
yanaendelea.
iii. Mgogoro kati ya Mjomba na Mama Suzi
Chanzo cha mgogoro huu ni Mjomba kumshauri Mama Suzi ampe elimu ya jinsia
na mahusiano binti yake. Mama Suzi anakataa na kusema kufanya hivyo ni
kuwafundisha watoto umalaya.
iv. Mgogoro kati ya Chausiku na Joti
Chausiku anamlaumu Joti kuwa anamahusiano na wasichana wengine,
anaendelea kulalama kuwa, hata zawadi anazompatia anawapatia wasichana
wengine. Chausiku anamtisha Joti kuwa atamchoma moto yeye na visichana
vyake. KICHEKO!!
Mgogoro wa nafsi
Huu ni mgogoro ambao humpata mhusika peke yake kati yake yeye na nafsi
yake.
- Suzi anapatwa na mgogoro wa nafsi pale anapopata mimba na kuambukizwa
virusi vya UKIMWI. Anabaki akilia, lakini hakujilaumu mwenyewe, bali
anamlaumu mama yake kwa kushindwa kumpatia elimu ya jinsia na mahusiano.
Katika ukurasa wa 40, anasema,
“Mimi na Joti tungepata bahati ya kuelimishwa tusingetumbu…”
Msimamo
Mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi. Katika tatizo la watoto wengi
kuangamia kwa ugonjwa wa UKIMWI, anashauri elimu ya jinsia na mahusiano
itolewe ili kuleta ukombozi kwa jamii.
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa elimu ya jinsia na mahusiano ikitolewa kwa watoto
itawasaidia kupambana na hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI.
KUFAULU NA KUTOKUFAULU KWA MWANDISHI
KUFAULU
Kufaulu katika fani
- Mwandishi ametumia lugha nyepesi inayoeleweka kwa urahisi.
- Mwandishi ametumia wahusika ambao wameibeba vizuri dhamira kuu
- Mwandishi ametumia muundo rahisi wa moja kwa moja ambao haumchoshi
msomaji wal a kumchanganya.
Kufaulu kwa maudhui
- Mwandishi amefaulu kufikisha dhamira katika jamii juu ya umuhimu wa
kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano.
- Pia mwandishi ameifungua jamii na kuionya juu ya hatari ya sayansi na
teknolojia endapo itatumiwa vibaya.
KUTOKUFAULU
Kutokufaulu katika fani
- Mwandishi ametumia mandhari ya mjini pekee kana kwamba maambukizi ya
virusi vya UKIMWI yanawakabili watoto waishio mjini tu.
Kutokufaulu katika maudhui
- Ugonjwa wa UKIMWI huwapata watu wote bila kuzingatia umri. Lakini
katika tamthiliya hii, wanaougua ugonjwa huu ni watoto pekee. Kwa kiasi
fulani mwandishi hajafaulu.
Hata hivyo kazi hii ni bora na inastahili pongezi kwa mafunzo makubwa
inayoyatoa katika jamii yetu iliyogubikwa na utandawazi.
Note! A free download pdf may contain a password, you have to join our groups
after downloading and ask for the documents password
uhakiki wa tamthiliya ya kilio chetu pdf download | dhamira katika tamthiliya ya kilio chetu pdf | Tamthiliya ya kilio chetu full movie download | kitabu cha kilio chetu kidato cha tatu pdf |
tamthiliya ya kilio chetu full movie | Tamthiliya ya kilio chetu video download | migogoro katika tamthiliya ya kilio chetu | kilio chetu sehemu ya kwanza | kilo chetu medical aid foundation | dhamira za kilio |
uchambuzi wa tamthiliya ya kilio chetu