pdf jinsi ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi ya Ualimu TAMISEMI pdf | Mfano wa barua za kazi ya ualimu pdf download |jinsi ya kuandika Barua ya maombi ya kazi kwa kiswahili pdf | Barua ya maombi ya kazi ya ualimu kwa kiingereza pdf dowmload
Related Posts
Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Fundi Umeme kwa Kiswahili
Simu: 0653 250 566,
Barua Pepe: milambo@gmail.com,
DAR ES SALAAM.
04/07/2022.
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Reli Tanzania,
S.L.P 76956,
DAR ES SALAAM.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA FUNDI UMEME
Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 30. Ninaomba Kazi ya Fundi Umeme
kama ilivyotangazwa na Shirika la Reli Tanzania siku ya tarehe
28/06/2022 katika Tovuti, mitandao ya Kijamii na mbao za matangazo.
Nina Cheti cha Fundi Umeme nilichotunukiwa kutoka VETA mwaka 2021. Pia,
nina uzoefu wa kufanya kazi na nimefanya kazi na Taasisi Ya 21st
Century Holding LTD.
Kutokana na elimu yangu, uwezo wa kufanya kazi nilionao, uzoefu, pamoja
na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi
hii. Endapo nitapata kazi hii ya Fundi Umeme, nitafanya kazi kwa bidii
kama ilivyoelekezwa. Baadhi ya majukumu yangu ni: kutengeneza mifumo ya
umeme, kuhakikisha vifaa vya umeme vinafanya kazi na kufuata maelekezo
nitakayopangiwa.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
____________
ISIKE MILAMBO
Barua ya Maombi ya Kazi ya Katibu mahsusi (yenye kumbukumbu namba)
Kuna matangazo hususani yale yanayotolewa na Serikali, humtaka mwombaji ataje kumbukumbu namba aliyoiona kwenye tangazo. Endapo hutaweka kumbukumbu namba kwenye barua ambayo umeelekezwa uweke, maombi yako yatapuuzwa. Tazama mfano na mahali Kumbukumbu namba inawekwa:
Mfano wa barua ya maombi ya kazi Katibu Mahsusi Daraja la III
Simu: 0653 250 566,
Barua Pepe: lumumba@gmail.com,
NJOMBE.
07/07/2022.
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji,
S.L.P 405,
MAKAMBAKO.
Kumb, Na:MTC/E.80/VOL I/47
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA KATIBU MAHUSUSI DARAJA LA III
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30. Ninaomba Kazi ya Katibu
Mahususi Daraja la III kama ilivyotangazwa na Halmashauri ya Mji
Makambako siku ya tarehe 27/06/2022 katika Tovuti, mitandao ya Kijamii
na mbao za matangazo.
Nina Cheti cha Katibu Mahsusi nilichotunukiwa kutoka Mafinga
Secretarial VETA, Iringa. Pia nina uzoefu wa kufanya kazi na nimefanya
kazi na Jimbo katoliki la Njombe. Pia, nimefaulu somo la hati mkato ya
Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja. Vilevile, nina
uzoefu wa kazi na nimefanya kazi na Halmashauri ya Mji Kigoma Ujiji.
Kutokana na elimu yangu, uwezo wa kufanya kazi nilionao, uzoefu, pamoja
na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi
hii. Endapo nitapata kazi hii ya Katibu Mahsusi Daraja la III, nitafanya
kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yangu yote. Baadhi ya majukumu yangu
ni: kuchapa barua na nyaraka za kawaida, kusaidia kupokea wageni na
kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wa kazi.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
____________
WEMA LUMUMBA
mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Tutorial Examination Officer II-Kiingereza
Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Udereva - Kiswahili
Simu: 0653 250 566,
Barua Pepe: daudmakoba@rocketmail.com,
DAR ES SALAAM.
14/06/2024.
Ofisi ya Rais,
Utumishi,
S. L.P 2320,
DODOMA.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA UDEREVA
Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 31. Ninaomba Kazi ya
Udereva kama ilivyotangazwa katika mbao za matangazo na mitandao
mbalimbali ya kijamii siku ya tarehe 13/06/2024.
Nina elimu ya kidato cha Nne na nimesoma katika shule ya Sekondari
Igunga na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2012. Nina uzoefu wa kazi hii na
nimefanya kazi na ‘Sumbawanga Limited’ kwa muda wa miaka
saba. Uzoefu wangu wa kazi ya udereva, umenifanya niwe bora katika kazi
hii na niweze kutimiza majukumu yangu yote kama vile kuhakikisha gari
ipo salama, kuendesha kwa kuzingatia kanuni zote za barabarani na
majukumu mengineyo. Ni matumaini yangu kwamba, sifa zangu hizi,
zinanifanya nistahili kupata kazi hii.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
_________
NJIKA MASUKE LONUNGU
Mfano wa barua ya maommbi ya Kazi ya Daktari Daraja la II
Simu: 0653 250 566,
Barua Pepe: daudmakoba@rocketmail.com ,
DAR ES SALAAM.
15/06/2024.
Mganga Mfawidhi,
Hospital ya Mkoa Katavi,
S.L.P 449,
MPANDA.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA DAKTARI DARAJA LA II
Mimi ni mwanamume Mtanzania mwenye umri wa miaka 38. Ninaomba
Kazi ya Daktari Daraja la II kama ilivyotangazwa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii.
Nina Shahada ya Udaktari niliyotunukiwa na chuo
kiitwacho European School of Medicine. Pia, nina uzoefu wa kazi na
nimefanya kazi na hospitali zifuatazo: Champion Hospital, Hospitali ya
Rufaa Iringa, na Heal Now Superspecialized Polyclinic.
Kutokana na uzoefu wangu, elimu, uwezo wa kufanya kazi nilionao pamoja
na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi
hii. Endapo nitapata kazi ninayoomba, nitafanya kazi kwa bidii na
kutimiza majukumu yangu yote ikiwemo kutoa uchunguzi na
matibabu.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
_________
MAHONA KIJA